Barcelona kuanza kibarua cha La Liga na Real Mallorca, Madrid dhidi ya Elbar

Ratiba ya ligi kuu nchini Hispania La Liga imetoka na mabingwa watetezi wa ligi hiyo Fc Barcelona wataanza kupepetana na Real Mallorca kufuatia ligi kusimama kwa zaidi ya miezi miwili kutokana na janga la virusi vya Corona.

Ligi Kuu Hispania ilisimama Marchi 12 ambapo Waziri Mkuu Pedro Sanchez ametoa ruhusa ya shughuli za kimichezo kuanza rasmi. Vinara wa ligi Barca watasafiri kwenda Mallorca Juni 13, siku mbili baada ya msimu kurudi kwa mtanange wa Sevilla kuvaana na Real Betis.

Real Madrid wako nyuma kwa alama mbili dhidi ya Barca wataanza michuano hiyo kwa awamu hii na mchezo wa nyumbani dhidi ya Elbar Juni 14. La Liga itakuwa ligi ya pili kurejea baada  ya kusitishwa kwa muda baada ya ligi ya Bundesliga ya Ujerumani kurudi mwezi Mei, EPL kukusudia kurudi Juni 17, kati ya zile ligi tano bora Ulaya huku ligi zote zikikusudiwa kuchezwa bila mashabiki.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends