Barcelona kwa mara ya kwanza kurudi uwanjani katika maandalizi ya kuendelea na msimu

56

Wachezaji wa klabu ya Barcelona wanarudi rasmi uwanja wa mazoezi hapo kesho Jumatano huku vipimo vya COVID-19 vikifanyika hapo hapo uwanjani kabla ya mazoezi ya mtu mmoja mmoja.

Mazoezi hayo yataanza kufanyika kwa kila mmoja kuwa pekee yake na baadae watafanya kwa vikundi kulingana na ruhusa itakayokuwa inatolewa na serikali.

Timu za La Liga zimepewa ruhusa ya kurudi mazoezi wiki hii kufuatia ruhusa ya serikali kupunguza vizuizi vya kubakia nyumbani na matembezi.

Zoezi la upimaji litakalofanyika kesho, wataalamu wa afya watafanya uchunguzi huo baada ya vifaa kuwekwa eneo la uwanja siku ya leo.

Ligi ya La Liga ilisimama tangu mwanzoni mwa mwezi Marchi ambapo pia Shirikisho la Soka nchini humo limekusudia kurejesha ligi hiyo mwezi Juni.

Raundi 11 zimesalia kutamatisha ligi hiyo huku Barca akiwa kinara wa ligi kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya Real Madrid.

Author: Bruce Amani