Barcelona mtegoni kwa Bayern Munich

Matumaini ya kikosi cha kocha Xavi Hernandez kucheza hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeendelea kuwa mseto kufuatia kulazishwa sare tasa na Benfica katika mchezo uliopigwa dimba la Camp Nou Jumanne.

Katika mechi hiyo, Barcelona walitengeneza nafasi takribani tatu muhimu za kupata goli lakini hawakuweza kuzitumia ukiachia mbali goli lililokataliwa la Ronald Araujo.

Baada ya matokeo hayo, Barcelona wanaendelea kushikilia nafasi ya pili kwenye msimamo wa Kundi alama mbili mbele ya timu iliyonafasi ya tatu Benfica nyuma ya kinara Bayern Munich na timu ya mwisho ni Dynamo Kyiv.

Mechi za mwisho zitachezwa Disemba 8, ambapo Barcelona watasafiri kwenda Allianz Arena nyumbani kwa Bayern Munich wakati Benfica watakuwa wanawakaribisha Kyiv.

Endapo Benfica watashinda kisha Barca watashindwa kuifunga Bayern, Barcelona watakuwa wameondolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2021/22 wataangukia kwenye Europa Ligi.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends