Barcelona na Real Madrid zaendeleza ubabe kileleni

281

Arturo Vidal alifunga bao la hovyo kabisa katika dakika za mwisho wakati vinara wa La Liga Barcelona wakitoka nyuma na kuwashinda washika mkia Leganes kwa mabao 2 – 1.

Youssef En-Nesyri alifunga bao safi katika dakika za mapema na kuwaweka Leganes kifua mbele wakati Barca wakihema kutafuta jibu.

Mabingwa hao waliimarika katika kipindi cha pili na Luis Suarez akasawazisha kupitia kichwa safi.

Bao la Vidal liliwaweka vinara hao kileleni mwa ligi dhidi ya mahasimu wao wa Real Madrid kwa faida ya mabao. Madrid walipata ushindi wa 3 – 1 dhidi ya Real Sociedad Barca na Madrid wana pointi 28 kila mmoja. Mabao ya Madrid yametiwa kimiani na Karim Benzema, Federico Valverde na Luka Modric. Willian Jose alikuwa ameiweka Sociedad kifumbe mbele katika dakika za mwanzo

Atletico Madrid wako katika nafasi ya tatu na pointi 24 baada ya kutoka sare ya 1 – 1 na Granada. Atletico wamecheza mechi moja zaidi ya wapinzani wao.

Author: Bruce Amani