‘Barcelona ni timu bora duniani’ – asema Aguero

412

Baada ya kukamilisha uhamisho wa kujiunga na miamba ya soka la Hispania Barcelona, mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Sergio Kun Aguero amesema klabu hiyo ni timu bora duniani.
Aguero alikamilisha uhamisho wa miaka miwili kutua Camp Nou kama mchezaji huru kufuatia mkataba wake kumalizika Juni 31 akihudumu kwa miaka 10 ndani ya Manchester City na sasa ni mchezaji rasmi wa Barcelona.
Akizungumza akiwa kwenye uzi wa wanacatalunya, Aguero amesema “kila mmoja anafahamu kuwa Barcelona ni klabu kubwa na bora duniani”.
“Nadhani nimefanya maamuzi sahihi katika maendeleo ya taaluma yangu ya kandanda, naamini nitaisaidia timu kushinda baadhi ya mataji hapa”. Aliongeza Aguero ambaye amewai kukitumikia kikosi cha Atletico Madrid.
Barcelona imeweka kipengele cha kutoka klabuni hapo kwa mshambuliaji huyo cha pauni milioni 86. Ameondoka Man City akiwa amefunga magoli 260 katika mechi 390, mechi ya mwisho ilikuwa dhidi ya Chelsea Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Author: Bruce Amani