Barcelona yaiadhibu Ferencvaros 5 – 1 dimbani Camp Nou

Klabu ya Barcelona imefanikiwa kuanza vyema kampeni ya kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya Uefa baada ya kuifunga Ferencvaros 5 – 1 mchezo ambao umepigwa dimba Camp Nou leo Jumanne. Wakati Barca inatoa adhabu hiyo, staa wa kikosi hicho Lionel Messi amefunga na kufikisha misimu 16 ya kucheza michuano hiyo mikubwa ngazi ya vilabu Ulaya.

Wakati huo huo kinda Pedri mwenye umri wa miaka 17 amefunga bao lake la kwanza akiwa na uzi wa Barcelona.

Messi alikuwa wa kwanza kutupia kwa penati, akafuatia kinda mwenye uwezo mkubwa hivi sasa Ansu Fati na kiungo mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho akaongeza la tatu, kabla ya Pedri na Dembele kuwahakikishia Wacatalunya hao ushindi.

Gerard Pique alionyeshwa kadi nyekundu kwa mchezo usio wa kiungwana kwa Ihol Kharatin, ambaye baada alikwamisha mpira nyavuni kwa tuta pia.

Author: Bruce Amani