Barcelona yaikaba Atletico Madrid kileleni La Liga kwa ushindi wa jioni dhidi ya Valladolid

Ushindi wa goli 1-0 wa Barcelona dhidi ya Real Valladolid mtanange wa Ligi Kuu nchini Hispania umeifanya timu hiyo kuwa nyuma kwa alama moja dhidi ya vinara Atletico Madrid katika msimamo wa La Liga.

Bao pekee kwenye mchezo huo limefungwa na winga wa kimataifa wa Ufaransa Ousmane Dembele akimalizia mpira wa Ronald Araujo katika dakika ya 90 ya mchezo huo.

Sasa Barca wako nyuma alama moja, hongera kwa kocha Ronald Koeman ambaye amekiongoza kikosi chake kushinda mechi sita mfululizo.

Matarajio ya ubingwa yatakuwa yamefufuka upya kwa Barcelona ambao umekuwa msimu wa kupanda na kushuka. Wamewakaribia Atletico baada ya wao kupoteza mechi dhidi ya Sevilla wikiendi, mechi ijayo ni El Clasico Barca watacheza na Real Madrid kabla ya kucheza Atletico Madrid mwezi ujao.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares