Barcelona yamfurusha kocha Ernesto Valvarde

53

Barcelona imempiga kalamu kocha Ernesto Valverde na kujaza nafasi na kocha wa zamani wa Real Betis Quique Setien.

Valverde, 55, aliisaidia Barca kubeba mataji mawili ya La Liga mfuulizo na sasa wanaongoza msimamo wa ligi kuu kwa tofauti ya mabao.

Hata hivyo, klabu hiyo ya Catalonia imekuwa na mfululizo wa matokeo na mchezo usioridhisha chini ya uongozi wa Valverde na kushindwa kufika fainali ya Champions League.

Setien, 61, aliiongoza Betis kumaliza msimu katika nafasi yao bora kabisa tangu mwaka wa 2005 na kutinga nusu fainali ya Copa Del Rey kabla ya kuondoka Mei mwaka jana. Amekubali kusiani mkataba wa miaka miwili na nusu uwanjani Camp Nou. Taarifa ya Barcelona imemshukuru Mhispania huyo kwa kazi yake nzuri.

Awali, kulikuwa na ripoti kuwa Barcelona inafanya mazungumzo na kiungo wao wa zamani Xavi Hernandez kuchukua nafasi ya Valverde.

Author: Bruce Amani