Barcelona yanasa saini ya Braithwaite

215

Barcelona imekamilisha dili la kumsajili mshambuliaji mpya katika dirisha dogo la dharura kutoka Leganes, Martin Braithwaite kwa dau la pauni milioni 18.

Usajili wa Barcelona umekuwa gumzo hivi karibuni kutokana na kusajili kipindi ambacho ligi zote kubwa zimemaliza usajili katika dirisha dogo la Januari.

Hilo linakuja kufuatia ruhusa maalumu ya La Liga kwa vilabu vyote kusajili mchezaji kwa shida maalumu.

La Liga kwenye kanuni zake wameweka kipengele cha klabu kusajili mchezaji mpya endapo mchezaji wa timu husika atapata majeruhi ya zaidi ya miezi tano na hivi sasa Dembele wa Barca atakaa nje ya uwanja kwa miezi sita.

Kandarasi ya Braithwaite itafikia tamati katikati ya mwezi Juni mwaka 2024.

TAKWIMU:

Amefunga goli 8 katika mechi 27 tangu ajiunge na Leganes huku goli sita zikiwa za Leganes nyingine ni za Middlesbrough.

“Tutapaza sauti zetu, hatuelewi chochote kuhusu kanuni hii, ni kanuni mbaya kwetu hasa wanapomchukua mchezaji aliyekuwa muhimu kwetu”. Alisema Mkurugenzi wa michezo wa Leganes akilaumu kile kilichotokea kwa mshambuliaji wao.

Ikumbukwe kuwa Leganes hivi sasa ipo katika mstari mwekundu kwenye msimamo wa kushuka daraja.

Author: Bruce Amani