Barcelona yashinda, Xavi avuna alama tatu

Kocha mpya Barcelona Xavi Hernandez ameanza vyema kampeni ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga baada ya mchezo wake wa kwanza kuvuna alama tatu muhimu mbele ya Espanyol kwa ushindi wa goli 1-0 mtanange uliopigwa dimba la Nou Camp.

Barcelona ambao walikuwa wananolewa na kocha Ronald Koeman kabla ya Xavi walipoteza nafasi nyingi za magoli kiasi cha kwamba wakajikuta hata mashabiki wanatoka upande wao.

Hata hivyo, ungwe ya pili kwa Xavi ilishuhudiwa kwa mara ya kwanza anashangilia bao ndani ya Barca kama kocha kufuatia goli la mshambuliaji Memphis Depay kwa njia ya penati.

Ushindi huo unaifanya Barcelona kukwea mpaka nafasi ya sita kwenye msimamo wa La Liga, ambapo mchezo ujao kwa Barca ni dhidi ya Benfica na wanahitaji kupata ushindi ili kufuzu kucheza hatua ya mtoano kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya mchezo utakaopigwa Jumanne Novemba 23.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends