Barcelona yatokea nyuma na kushinda mbele ya Valencia, Messi atupia mbili

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Lionel Messi amehusika katika ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Valencia baada ya kufunga goli mbili mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga uliopigwa Jumapili.

Barca walilazimika kutokea nyuma kufuatia goli ya mapema ya mchezaji wa zamani wa Arsenal Gabriel kisha Messi akakosa penati kabla ya kumalizia.

Antoine Griezmann alianza kuipa uongozi Barca kabla ya Messi kupiga freekick ya aina yake na Carlos Soler kuwapa matumaini Valencia kwa goli lake.

Barcelona watacheza dhidi ya vinara Atletico Madrid Jumamosi katika dimba la Camp Nou.

Licha ya ushindi huo bado Barca wanabakia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Hispania nyuma ya Real Madrid na vinara wenyewe Atletico Madrid. Barca na Madrid wana pointi 71 kila mmoja wakati Atletico wana pointi 73.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares