Batambuze kujiunga na Gor

Mchezaji wa kimataifa wa Uganda Shafik Batambuze anatarajiwa kujiunga na klabu ya Gor Mahia ya Kenya kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu.

Batambuze kwa sasa hana timu baada ya kuichezea Singida United ya Tanzania msimu uliopita.

Mtendaji mkuu wa Gor Mahia Lodvick Aduda ameviambia vyombo vya habari nchini Kenya kwamba Batambuze na mchezaji mwingine  Kenneth Muguna watajiunga na timu hiyo Januari mwakani.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends