Bayern Munich waanza mahesabu walipoishia Ligi ya Mabingwa, waichakaza Atletico Madrid 4 – 0

449

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Bayern Munich wameendeleza kasi na kiwango bora walichokuwa nacho msimu uliopita 2019/20 baada ya Jana Jumatano kuwaadhibu Atletico Madrid goli 4-0 katika mtanange uliopigwa dimba la Allianz Arena.

Ushindi huo unaifanya Bayern ambayo ni mabingwa wa Bundesliga na Kombe la Dunia ngazi klabu kufikisha mechi 12 bila kupoteza kwenye mashindano ya Ulaya.

Ni siku 59 pekee tangu walipotwaa taji hilo Jijini Lisbon 2020, kikosi cha kocha Hansi Flick kilikuwa na ubora mkubwa kuliko cha Diego Simeone ambapo magoli mawili ya winga Kingsley Coman, Leon Goretzka na Corentin Tolisso yaliwapa ushindi mnono kabisa dhidi ya washiriki wa robo fainali msimu uliopita Atletico Madrid.

Author: Bruce Amani