Bayern Munich wamnyakuwa kocha Nagelsmann kutoka RB Leipzig

Mabingwa wa Ligi Kuu nchini Ujerumani Bayern Munich wametangaza kuwa mwishoni mwa msimu huu kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann atajiunga na klabu hiyo kwa kandarasi ya miaka mitano.

Bosi wa sasa wa Bayern Hans Flick itakumbukwa wiki iliyopita aliomba kuondoka klabuni hapo baada ya mafanikio makubwa kwa kipindi kifupi.

Nagelsmann katika umri wa miaka 33, anatajwa kama miongoni mwa makocha wenye umri mdogo lakini uwezo mkubwa kufuatia kukiongoza vyema kikosi cha RB Leipzig.

Akizungumzia ujio wake Rais wa Bayern Munich Herbert Hainer amesema Julian Nagelsmann atasimamia timu kwa kipindi kijacho.

Ataanza kazi rasmi Julai Mosi, 2021 ambapo imeelezwa kuwa Munich wametoa kiasi ya pauni milioni 20 kama fidia ya mkataba.

“Nitaondoka RB Leipzig kwa huzuni kubwa lakini upendo wangu utakuwa hapa daima”. Kukinoa kikosi cha Bayern Munich ni hatua kubwa maishani mwangu”, alisema Nagelsmann.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares