Bayern Munich yaitwanga Lazio 3-1 na kutinga robo fainali Ligi ya Mabingwa

167

Bayern Munich imetinga hatua ya robo fainali baada ya kuifunga Lazio kwa goli 2-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mtanange uliopigwa Jana Jumatano.

Mshambuliaji wa Bayern Robert Lewandowski alikuwa kwenye karatasi ya wafungaji akipachika bao kwa njia ya penati kabla ya bao la pili lililofungwa na Eric Maxim.

Strika huyo Lewandowski raia wa Poland alikwamisha mpira nyavuni baada ya Leon Goretzka kufanyiwa faulo na Francesco Acerbi.

Akiingia kutokea bechi, Eric Maxim Choupo-Moting alifanya 2-0, Lazio walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa Marco Parolo.

Matokeo ya jumla yanakuwa 6-2 katika mchezo wa mikondo miwili.

Author: Bruce Amani