Bayern Munich yaondoa ofa ya mkataba mpya kwa staa wake David Alaba

Mshindi mara mbili wa Champions League David Alaba anaelekea kuondoka klabu hiyo baada ya miamba hao kusema kuwa mazungumzo kuhusu mkataba mpya yamevunjika. Mkataba wake unakamilika mwishoni mwa msimu huu.

Rais wa klabu hiyo Herbert Hainer amenukuliwa na chombo kimoja cha habari Ujerumani akisema kuwa Bayern iliweka mwishoni mwa Oktoba kuwa muda wa mwisho kwa Muastria huyo na wakala wake kujibu ofa nzuri kabisa ya mkataba mpya, na baada ya muda huo kuisha bila makubaliano, ofa hiyo ikaondolewa.

“Baada ya hapo tuliamua kuondoa kabisa ofa hiyo mezani. Hiyo ina maana hakuna ofa nyingine ndefu.” Amesema Hainer.

Alaba anayeweza kucheza kama mlinzi au kiungo ameichezea Bayern mechi 271 tangu alipojiunga nao kama mchezaji chipukizi mwaka wa 2008. Ameshinda mataji tisa ya Bundesliga. Mkataba wake unakamilika mwishoni mwa msimu huu.

Reuters, AFP, AP, DPA

Author: Bruce Amani