Bayern Munich yarudi njia za ushindi, yaitwanga Lazio 4-1 Ligi ya Mabingwa

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya klabu ya Bayern Munich wameanza kwa kishindo hatua ya 16 bora baada ya kuitandika Lazio bao 4-1 ugenini mchezo uliopigwa Leo Jumanne Februari 23, 2021.

Bayern ambao walikuwa kwenye kipindi kigumu cha kuangusha alama katika mechi mbili za nyuma ikiwemo ya Bundesliga walikuwa wanahitaji ushindi ili kurejesha hali ya kujiamini kwa wachezaji.

Bao la kwanza la Bayern limefungwa na Robert Lewandowski, kabla ya Jamal Musiala, Leroy Sane kuongeaza mengine na Francesco Acerbi akatumbukiza Mpira kwenye lango lake kabla ya Lazio kutokea Italia kupata bao moja pekee la kufutia machozi kupitia kwa Joaquim Correra.

Kabla ya mchezo, kocha Hans Flick alisema anahitaji kuwaona wachezaji wakirudi kwenye ubora na kupata matokeo chanya dhidi ya Lazio.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares