Bayern Munich Yatandikwa na Bochum 4-2 Bundesliga

197

Bochum imeiduwaza Bayern Munich kwa kuichapa bao 4-2 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ujerumani. Kwenye mechi HIYO, goli zote nne zilifungwa ungwe ya kwanza kwa mara ya kwanza tangia mwaka 1975.

Bochum magoli yake yakifungwa kupitia kwa Christopher Antwi-Adjei likiwa ni bao la kusawazisha baada ya Bayern kutangulia kupata bao la Robert Lewandowski.

Magoli mengine yakafungwa na Jurgen Locadia, Cristian Gamboa na Gerrit Holtmann ambapo kipindi cha pili bao la pili la Bayern likitupiwa na Lewandowski.

Kinakuwa kipigo cha kwanza kwa Bayern katika mechi 22 zilizopita za Ligi Kuu Ujerumani Bundesliga ambapo sasa wanakuwa kileleni mwa msimamo wa Bundesliga kwa tofauti ya alama tisa dhidi ya timu iliyo nafasi ya pili Borussia Dortmund ambao wana mchezo Leo Jumapili na Union Berlin.

Kwa upande wa Bochum wanakamata nafasi ya 11 kwenye msimamo huo.

Author: Bruce Amani