Bayern waanza mzunguko wa pili wa msimu na ushindi

56

Bayern Munich wameanza mzunguko wa pili wa msimu kwa kuonyesha mchezo imara na kuwazidi nguvu Hoffenheim kwa kuwafunga mabao sawa na walivyofanya katika siku ya kwanza ya msimu.

 

Timu hiyo ya kocha Niko Kovac iliutawala mchezo katika kipindi cha kwanza baada ya kupoteza nafasi kadhaa kabla ya Leon Goretzka kufunga. Robert Lewandowski alipiga kichwa kilichookolewa na kipa Oliver Baumann lakini Goretzka akawa mwepesi wa kusukuma wavuni bao.

Baadaye kiungo wa zamani wa Schalke aliweka wavuni bao la pili. Bayern walipiga counter kali sana ambapo Goretzka kumalizia shambulio hilo la kushtukiza.

Bayern walipoteza ukakamavu katika kipindi cha pili na kwa mara ya pili katika mchezo huo, bao lilipatikana katika mkwaju wa kona.  Hoffenheim  waliondosha kona, Joelinton alimpa pasi Leonardo Bittencourt ambaye aliupiga mpira mrefu hadi kwake Nico Schulz. Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani alisukuma wavumi bao safi sana la kuunganisha mpira

Manuel Neuer aliokoa bao kutoka kwa Adam Szalai wakati Hoffenheim walijaribu kutafuta bao la pili kabla ya Lewandowski kufunga bao la tatu baada ya move ilioanzishwa na Joshua Kimmich.

“Kipindi cha kwanza kilikuwa bora zaidi,” Niko Kovac aliiambia televisheni ya ZDF baada ya mechi, kabla ya kuongeza kuwa huo ndo aina ya mchezo aliotarajia kutoka kwa timu yake na alijua timu yake inaweza kuuonyesha. Matokeo hayo yanaiacha Bayern pointi tatu nyuma ya vinara Borussia Dortmund, watakaocheza na RB Leipzig Jumamosi.

Author: Bruce Amani