Bayern wabeba taji la saba la Bundesliga mfululizo

60

Bayern Munich wametawazwa mabingwa wa Ujerumani kwa msimu wa saba mfululizo baada ya kuwasaga Eintracht Frankfurt 5 – 1 katika siku ya mwisho ya msimu.

Timu hiyo ya kocha Niko Kovac, ambao walikuwa nyuma ya vinara Borussia Dortmund na pengo la pointi tisa baada ya mechi 12, walihitaji sare tu ili kunyakua taji lao la 12 la  Bundesliga. Kingsley Coman alifungua mvua ya mabao kabla ya Sebastian Haller kusawazisha. Kisha David Alaba, Renato Sanches, Franck Ribery na Arjen Robben wakaihakikishia Bayern ushindi dimbani Allianz Arena

Walimaliza pointi mbili mbele ya Borussia Dortmund ambao walishinda 2 – 0 dhidi ya Borussia Moenchengladbach mabao yakifungwa na Jadon Sacho na Marco Reus.

Manguli wa Bayern Arjen Robben na Frank Ribery walifunga bao moja kila mmoja katika mechi yao ya mwisho katika uwanja wa nyumbani. Mikataba yao inamalizika msimu huu. Wote wawili ambao walicheza misimu 22 na kufunga mabao 185 na kubeba mataji 15, walianzia mechi kenye benchi pamoja na beki Rafinha ambaye pia anaondoka msimu huu

Author: Bruce Amani