Bayern watengeneza pengo la alama saba kileleni Bundesliga, wawachapa Leipzig 1-0

Bayern Munich wamekwea mpaka alama saba kileleni baada ya kuitandika RB Leipzig bao 1-0 na sasa wanalichuchumilia taji la 9 mfululizo la Ligi Kuu nchini Ujerumani – Bundesliga.

Bao pekee limefungwa na Leon Goretzka akimalizia mpira wa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Thomas Mueller.

Bayern Jumatano wataendelea na kampeni yao ya kutetea taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris St-Germain robo fainali.

Bayern ambao inamkosa mfungaji wao Robert Lewandowski kutokana na majeruhi ya goti watakutana na Union Berlin Jumamosi ijayo wakati Leipzig watacheza na Werder Bremen.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares