Bayern yaibomoa Hertha na kukaribia Leipzig

Mabingwa watetezi wa Bundesliga Bayern Munich imefanikiwa kuibuka na ywa goli 4-0 dhidi ya Hertha Berlin ushindi unaoipa nafasi kupanda mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Ulikuwa mwanzo mzuri kwa kocha Jurgen Klinsmann baada ya kuwazuia kufunga hata goli moja Bayern dakika zote 45 kabla ya kukubali kuruhusu goli 4 kipindi cha pili, magoli yaliyofungwa kupitia Thomas Muller, Robert Lewandowski(pen), Thiago Alcantara kabla ya nyota wa mchezo huo Perisic kumalizia goli la 4.

Matokeo yanaikweza vyema, sasa Bayern Munich imekuwa alama nne nyuma ya vinara RB Leipzig.

Siku ya Jumamosi, vinara RB Leipzig walishinda goli 3-1 dhidi ya Union Berlin na kuendelea kung’ang’ania nafasi ya kwanza, Marius Bulter alianza kuipa uongozi Union kabla ya Marcel Sabitzer na Timo Werner kufunga na kuipa Leipzig alama zote tatu.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends