Bayern yaingia hofu, Lewandowski, Gnabry kuikosa PSG

Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Bayern Munich wanaweza kumkosa winga wao Serge Gnabry katika mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Paris St-Germain kutokana na shida katika shingo yake.

Bayern, ambao wako kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Ujerumani Bundesliga kwa tofauti ya alama saba, mapema wiki iliyopita waliweka wazi kuwa mshambuliaji Robert Lewandowski na kiungo Marc Roca watakuwa nje ya uwanja kwa takribani mwezi mmoja.

Bado haijawekwa wazi kama Gnabry atakosa mechi hiyo au la, hata hivyo winga wa zamani wa Manchester City Leroy Sane anaweza akavaa viatu vyake.

Kwa upande wao PSG watakosa huduma ya Alessandro Florenzi na Marco Verratti kufuatia vipimo vya Covid-19 kuonyesha kuwa na viashiria vyake wiki iliyopita.

Staa wa Brazil Neymar Jr na winga wa Ufaransa Kylian Mbappe wataongoza safu ya ushambuliaji.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares