Bayern yainyeshea Stuttgart na kupunguza mwanya na Dortmund

Mabingwa Bayern Munich walilazimika kufanya kazi kubwa kwa zaidi ya saa moja kabla ya kuibwaga VfB Stuttgart 4-1 katika Bundesliga Jumapili na kubaki katika nafasi ya pili pointi sita nyuma ya vinara Borussia Dortmund.

Bayern, ambao watakabana koo na Liverpool katika Champions League hatua ya 16 mwezi ujao, ilipata bao la kwanza kupitia Thiago Alcantara.

Stuttgart walisawazisha katika dakika ya 26 kupitia Tasous Donis kabla ya Christian Gentner kujifunga bao katika lango lao, kupitia mkwaju wa Serge Gnabry na kuwapa tena Bayern uongozi.

Mshambuliaji wa Bayern alipoteza penalty kwa kupiga besela katika dakika ya 65 lakini Leon Goretzka alifunga kichwa dakika 20 kabla ya mechi kumalizika likiwa bao lake la tano msimu huu. Lewandowski kisha akarekebisha makosa yake ya  kukosa penalti kwa kufunga bao la nne na la ushindi mnono ambao uliwaweka katika nafasi ya pili na pointi 42.

Dortmund wana pointi 48 wakati Borussia Moenchengladbach wakiwa na 29 katika nafasi ya tatu.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends