Bayern yakamata usukani kwa kishindo, Leipzig yayumba

Bayern Munich imetua kwa kishindo kileleni mwa ligi kuu ya kandanda Ujerumani – Bundesliga baada ya ushindi wa mabao 3 kwa moja dhidi ya Mainz hapo jana. RB Leipzig wangeweza kuikamata tena nafasi ya kwanza katika mechi iliyochezwa baadaye jana lakini ikatoka sare ya mabao 2 – 2 na nambari nne Borussia Moenchengladbach baada ya kujikuta wakiwa nyuma 2 – 0. Mabingwa Bayern sasa wanaongoza msimamo wa ligi na pengo la pointi moja wakiwa na 42 baada ya kucheza mechi 20. Borussia Dortmund waliwafunga Union Berlin 5 – 0 katika mechi ambayo mchezaji wao mpya chipukizi Erling Braut Haaland alifunga mabao mawili. Leverkusen inayoshikilia nafasi ya tano ilifungwa mabao 2 – 1 na Hoffenheim.

Author: Bruce Amani