Bayern yapigiliwa msumari wa 2-1 na Eintracht Frankfurt na kuziweka tena wazi mbio za ubingwa wa ligi

Bayern Munich wamekutana na kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa Eintracht Frankfurt katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Ujerumani Bundesliga na kupoteza nafasi ya kuwa kileleni kwa tofauti ya alama nane.

Daichi Kamada na Amin Younes waliipa uongozi timu mwenyeji kabla ya mapumziko. Bayern Munich ambao ni mabingwa wa Kombe la Dunia ngazi ya wakarudi mchezoni katika ngwe ya pili kupitia kwa Roberto Lewandowski aliyemalizia mpira wa Leroy Sane.

Kikosi cha kocha kijana Julian Nagelsmann cha RB Leipzig kinaweza kupunguza pengo la pointi kufikia mbili endapo kitaibuka na ushindi kwenye mechi ya kesho Jumapili dhidi ya Hertha Berlin.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares