Bayern yarejea kwa kishindo dhidi ya Cologne, Leipzig yatawala

51
Rafiki na goli. Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski amekiongoza kikosi cha Munich kushinda mchezo wa Bundesliga kwa goli 4-0 dhidi ya Cologne kwenye mchezo wa ligi hiyo.
Lewandoswki hivi sasa anafikisha goli 9 ndani ya mechi 5 za Bundesliga huku akiwa sehemu ya wafungaji kwenye mchezo wa Uefa Champions League dhidi ya Red Star Belgrade.
Mbali na goli mbili za Lewandoski, nyota mpya ndani ya Bavaria Philippe Coutinho alifunga goli la kwanza ndani ya Munich kwa njia ya penati.
Goli la mwisho la Bayern Munich likifungwa pia na mchezaji mpya Ivan Perisic.
Baada ya wiki mbaya kwa Bayern kwani walianza kutoa sare dhidi ya RB Leipzig kisha zikaibuka tetesi kuwa Niko yupo mbioni kuondoshwa kufuatia matokeo mabaya huenda mambo yametulia.
Matokeo mengine.
Bayer Leverkusen 2-0 Union Berlin
Hertha Berlin 2-1 Paderborn
Freiburg 1-1 Augsburg
Werder Bremen 0-3 Leipzig
Msimamo wa ligi hiyo bado utakuwa chini ya RB Leipzig baada ya kuendelea kufanya vizuri katika michezo hii ya awali.

Author: Bruce Amani