Bayern yatoa adhabu kali kwa Bremer SV ya bao 12-0

Klabu ya Bayern Munich imeitandika bao 12-0 klabu ya Bremer SV inayoshiriki Ligi daraja la tano mchezo wa Kombe la Ujerumani hatua ya kwanza, huku mshambuliaji wa Cameroon Eric Maxim Choupo-Moting akiingia kambani mara nne.

Choupo-Moting alifunga goli la kuongoza baada ya dakika nane kabla ya Jamal Musiala kuingia kambani na karamu ya magoli ikaendelea ambapo alifunga Leroy Sane, Michael Cuisance, Bouna Sarr, Corentin Tolisso na lile bao la kujifunga la Malik Tillman.

Ushindi huo unakuwa wa kwanza kwa Bayern Munich tangia mwaka 1997 katika mwaka huu walishinda bao DJK Waldberg 16-1.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends