Bayern yatolewa jasho katika ushindi dhidi ya Cologne

Bayern Munich imefanikiwa kupata matokeo chanya ya 3-2 mbele ya Cologne katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga, huku Serge Gnabry akiingia kambani mara mbili.

Kama kawaida, Robert Lewandowski alifungua bao la uongozi akitumia vyema pasi ya Jamal Musiala kunako dakika ya 50, kabla ya nyota wa zamani wa Arsenal Gnabry kuongeza bao lingine.

Ingawa baadaye wageni Cologne walionekana kurudi kwa nguvu na kupata goli mbili za haraka kupitia kwa Anthony Modeste na Mark Uth.

Kunako dakika za jioni, Gnabry akafunga bao lingine kwa shuti kali ndani ya boksi na kuandikisha ushindi huo.

Lewandowski ameendelea kuandikisha rekodi kufuatia kufunga goli kwenye mechi 12 za Bundesliga ambapo katika mechi hizo amefunga jumla ya bao 19, mara ya mwisho kutofunga ndani ya Bayern ilikuwa mwezi Februari.

Pia ni ushindi wa kwanza kwa kocha Julian Nagelsmann baada ya mechi ya awali kumalizika kwa sare kwa Borussia Monchengladbach.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends