Beckenbauer anatamani kumuona Klopp akikamata usukani Bayern

Mchezaji  nguli  wa  kandanda  wa  Ujerumani  Franz Beckenbauer  amesema  kwamba  anataka  kumuona  kocha  wa  Liverpool  Juergen Klopp katika  benchi  la  ufundi la Bayern.

Wakati  Ujerumani  ikisherehekea  mafanikio  ya  Klopp  katika  Champions League  siku  ya  Jumamosi, Beckenbauer  ameliambia  gazeti maarufu Ujerumani la  Bild  kwamba  anataka  sana  kumuona  kocha  huyo wa  zamani  wa  Borussia  Dortmund  akijiunga  na  mabingwa  wa  Bundesliga, Bayern Munich.

“Sitaka  kitu  kingine  zaidi  ya  kumuona  Klopp akija  Bayern siku  moja, kitakuwa  kitu  kizuri  sana,” amesema  Beckenbauer mwenye  umri  wa  miaka  73, ambaye  alishinda  ubingwa  mara tano wa Bundesliga  na  Bayern  akiwa  kama  mchezaji  na  kocha. Ubingwa wa  kwanza  wa  Klopp  wa  Champions League ulisababisha  sherehe  kubwa  katika  vyombo  vya  habari  za  michezo  nchini Ujerumani.

Author: Bruce Amani