Beckham amvuta Higuain Inter Miami

Mshambuliaji wa Argentin Gonzalo Higuain ameachana na miamba ya soka la Italia Juventus baada ya mkataba wake kusitishwa kwa makubaliano maalumu.

Strika huyo wa zamani wa Real Madrid na Chelsea anatarajiwa kujiunga timu inayomilikiwa na David Beckham ya Inter Miami ya Marekani.

Higuain mwenye umri wa miaka 32 alijiunga na Juventus akitokea Napoli mwezi Julai mwaka 2016 kwa ada iliyoweka rekodi ya pauni milioni 75.

Katika kipindi hicho, alikuwa miongoni mwa wachezaji walionunuliwa kwa gharama kubwa kati ya watatu mwaka huo 2016.

Wiki iliyopita Higuain alisalimiwa na miongoni mwa wamiliki wa timu ya Miami anayefahamika kwa jina la Jorge Mas, timu ya Miami inamilikiwa na watu wanne, nahodha wa zamani wa England David Beckham ni miongoni mwa.

Higuain alifunga goli 66 katika mechi 149 ambapo amekitumikia kikosi cha AC Milan na Chelsea lakini bado alikuwa mtumishi mwema wa Juventus.

Ujio wa kocha mpya wa Juventus umeondoa uwezekano wa staa huyo kuendelea kubakia Turin, Andrea Pirlo alitangaza kuachana na mshambuliaji huyo.

“Alikuwa mchezaji bora sana, alikuwa mwema kwetu lakini muda wa kuendelea kuwa naye umeisha”. Alisema Pirlo.

Author: Bruce Amani