Beki Laporte acheza mechi ya kwanza ndani ya uzi wa Hispania

Beki wa kati wa Manchester City Aymeric Laporte amecheza mechi ya kwanza kwenye uzi wa taifa la Hispania katika mchezo wa kupasha misuli dhidi ya Ureno kuelekea Euro 202 mbele ya mashabiki 14,743 dimbani Wanda Metropolitano.
Kitasa huyo mwenye umri wa miaka 27, alipewa uraia wa Hispania badala ya Ufaransa kutokana na kutocheza mechi yoyote ngazi ya wakubwa kwa Ufaransa.
Nafasi ya kipekee kwenye mechi hiyo iliyoishia sare tasa ilipotezwa na Alvaro Morata aliyegongesha mwamba, huku Ferran Torres pia akipoteza nafasi.
Ureno walikosa ushindani ambapo walipata kulenga goli mara moja kupitia mpira wa kichwa wa Danilo Pereira.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares