Beki wa England na Atletico Madrid Trippier afungiwa wiki 10 kwa kukutwa na makosa ya kubeti

192

Mlinzi wa pembeni wa klabu ya Atletico Madrid na timu ya taifa ya England Kieran Trippier amefungiwa wiki 10 kujihusisha na shughuli za soka duniani pamoja na adhabu ya pauni 70,000 baada ya kukiuka kanuni za kubeti.

Chama cha Soka nchini England kimemkuta na makosa hayo baada ya uchunguzi ambao ulianza kufanywa mwaka 2019 hata kabla ya mlinzi huyo kuondoka Tottenham na kujiunga na Atletico.

Beki huyo mwenye umri wa 30 amekana madai ya kukiuka kanuni hizo lakini makosa manne yamethibitishwa kuwa ni kweli alifanya wakati anasikilizwa.

Adhabu hiyo inaanza kutekelezwa mara moja. Atakosa mechi 12 za La Liga kwa vinara Atletico, ukijumulisha na mechi za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Chelsea Februari 23 ingawa atakuwepo mechi ya dabi dhidi ya Real Madrid Machi 7.

Author: Bruce Amani