Benin mdomoni mwa Morocco 16 bora

Miamba ya milima ya Atlas Morocco itacheza na Benin leo Ijumaa katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Kimataifa Afrika Afcon 2019 inayofanyika nchini Misri, mtanange utakaochezwa majira ya saa 1jioni masaa ya Afrika Mashariki.

Morocco wanaingia hatua hii wakiwa na kumbukumbu ya michuano ya mwaka 2017 ambapo waliondolewa katika robo fainali dhidi ya Misri. Licha ya kupoteza mwaka huo ambapo Cameroon alitwaa taji lile msimu huu anakutana na ladha tofauti katika ngazi ya ushindani.

Taifa la Morocco ni miongoni mwa Mataifa yanayopigiwa upatu kubeba taji la Afcon 2019, ikiwa imeshinda michezo yote mitatu ya hatua ya makundi dhidi ya timu ngumu kama Ivory Coast, Afrika ya Kusini na Namibia. Huku ikiwa haijabeba taji la Afcon tangu mwaka 1976.

Kwa upande wa Benin ni timu dhaifu kulinganisha na Morocco hata kwenye kundi F imepita kama “Best Loser” timu iliyopita kwa utofauti ya mechi za kufungwa na kufunga. Benin imeingia hatua hii kutoka kwenye kundi la Cameroon na Ghana.

Mshindi wa mchezo huo tacheza dhidi ya mshindi wa Uganda dhidi ya Senegal katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Author: Asifiwe Mbembela

Facebook Comments