Benzema kusalia Real Madrid mpaka 2023

Nahodha wa Real Madrid Karim Benzema amekubali kumwaga wino wa kuendelea kukitumikia kikosi cha Los Blancos mpaka mwaka 2023.

Mkataba wa Benzema wa awali ulikuwa unaelekea mwishoni, kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja utamfanya kuitumikia timu hiyo miaka 14.

Benzema, 33, alijiunga na miamba ya soka la Hispania 2009 akifunga bao 281 kwenye miaka 12 ndani ya klabu hiyo misimu mitatu iliyopita zaidi ya bao 20.

Benzema raia wa Ufaransa ni mchezaji wa tano ndani ya Real Madrid mwenye goli nyingi zaidi, anakuwa mchezaji wa pili kumwaga wino baada ya mlinda mlango Thibaut Courtois.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends