Berkane kuvaana na Zamalek mkondo wa kwanza wa fainali

Mechi ya mzunguko wa kwanza wa fainali ya kuwania taji la Shirikisho barani Afrika kati ya RS Berkane ya Morocco na Zamalek ya Misri inachezwa Jumatatu 20.05.2019.

Mechi hiyo itachezwa katika uwanja wa Stade Municipal de Berkane, mjini Berkane.

RS Berkane ilifika katika hatua hii baada ya kuishinds CS Sfaxien ya Tunisia katika mechi ya nusu fainali huku Zamalek ikiishinda Etoile du Sahel.

Mwamuzi wa kesho ni Mzambia Janny Sikazwe. Mechi ya marudiano itakuwa wiki ijayo katika uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.

Lakini fainali ya kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika, mechi ya kwanza, itachezwa Ijumaa ijayo kati ya Wydad Casablanca ya Morocco na Es Perance de Tunis.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends