Berkane, Zamalek kuumana fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika

Klabu ya Renaissance Berkane ya Morocco na Zamalek ya Misri zimetinga katika fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika CAF baada ya kuziondoa klabu za Tunisia CS Sfaxien na Etoile Sahel. Wakiwa katika uwanja wa nyumbani, Berkane waliwaduwaza washindi mara tatu CS Sfaxien mabao 3 -0 katika nusu faianali mkondo wa pili na kufuzu katika fainali kwa jumla ya mabao 3 – 2.

Nayo Zamalek ilipenya kufuatia ushindi wa jumla wa 1 – 0 baada ya kutoka sare tasa na Etoile Sahel. Berkane ambao watashiriki fainali ya Kombe la Afrika kwa mara yao ya kwanza, watawaalika Zamalek katika mkondo wa kwanza nchini Morocco mnamo Mei 19 huku mechi ya mkondo wa pili ukiwa nchini Misri siku saba baadaye. Zamalek, ambao wameshinda mataji tisa ya CAF, wanatumaini kumaliza ukame wao wa kusubiri taji la Afrika kwa miaka 1

Author: Bruce Amani