Biashara United yajiandaa kuipeperusha bendera ya Tanzania

Biashara United inaendelea na mazoezi yakujiweka sawa kabla ya mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika raundi ya pili mkondo wa kwanza dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya, mtanange utakaopigwa dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuanzia saa tisa mchana.

Maandalizi ya Biashara United yanafanyika kwenye viwanja vya Karume Jijini Dar es Salaam ambapo wanakusudia kusafiri kuelekea Libya siku chache baada ya mchezo huo kuelekea mtanange wa mkondo wa pili Kombe la Shirikisho.

Biashara United imefika hatua hiyo baada ya kuiondoa Dikhil ya Djibouti raundi ya kwanza.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends