Bila Conte, Lukaku, Inter yaichapa Genoa Serie A

Inter Milan wameanza kibabe kampeni ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu nchini Italia kwa kuichapa bao 5-0 Genoa katika mchezo uliopigwa dimba la San Siro Leo Jumamosi Agosti 21.

Inter ikiwa na kocha mpya Simone Inzaghi pamoja na mshambuliaji mpya Eden Dzeko ilianza kupata goli kupitia kwa Milan Skriniar kwa kichwa, kabla ya Hakan Calhanoglu kuongeza lingine na mshambuliaji Edin Dzeko’s kufunga bao la tatu.

Arturo Vidal na Dzeko walifunga ungwe ya pili na kufanya matokeo kuwa tano kwa nunge jambo linaloashiria pengo la Conte wala Lukaku kwa hapa mwanzoni sio tatizo tena

Licha ya kumkosa Lautaro Martinez bado, Mabingwa inter walifanikiwa kuondoka na alama tatu zote huku Genoa wakiambulia patupu.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends