Bila Harry Kane hakuna tatizo, Tottenham yatoa kichapo kwa Man City

Licha ya kumkosa mshambuliaji wa kimataifa wa England Harry Kane, klabu ya Tottenham imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England Manchester City mchezo wa ufunguzi wa Ligi hiyo.

Mtanange huo umepigwa Leo Jumapili Agosti 15 huku Manchester City ikikosa huduma ya kiungo mshambuliaji Kevin de Bruyne na Phil Foden huku wakimtumia kiungo mshambuliaji wa zamani wa Aston Villa Jack Grealish

Bao pekee kwenye mchezo huo limefungwa na winga Son Heung-Min ambaye alimpa kocha Nuno Espirito Santo ushindi wa kwanza kwenye Ligi katika mechi ya kwanza pia baada ya kumpita mlinda mlango Ederson.

Kane amekosa mchezo huo kutokana na uvumi kuwa bado dili lake la kujiunga na Man City halijawekwa bayana ambapo Mwenyekiti wa klabu Levy anapinga kuondoka kwake.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends