Bingwa mtetezi wa Carabao Man City apangwa na Oxford United robo fainali

364

Mabingwa watetezi wa Kombe la Carabao Manchester City wamepangwa kucheza dhidi ya timu ya daraja la pili Oxford United katika hatua ya robo fainali ya kimbembe hicho.

Klabu ya Colchester United, imekutana na droo ya kwenda dimba la Old Trafford kucheza dhidi ya Manchester United ambayo ni mabingwa mara tano wa michuano ya Ligi.

Timu iliyopanda daraja msimu huu EPL, Aston Villa watakutana na mabingwa mara nne Liverpool, huku Everton wakiwa nyumbani dhidi ya Leicester City.

Kibembe cha ratiba ya robo fainali imekusudiwa kupigwa kuanzia wiki ya Disemba 16 mwaka huu.

Licha ya ratiba hiyo kuonyesha hivyo lakini Liverpool huenda ratiba yake ikapanguliwa upya baada ya ratiba yake ya mwezi huo kuonyesha Majogoo wa jiji la Liverpool watakuwa na katika kalenda ya FIFA kucheza Kombe la Dunia ngazi ya vilaby Disemba 18.

Robo fainali imepangwa hivi:-

Oxford United v Manchester City

Manchester United v Colchester United

Aston Villa v Liverpool

Everton v Leicester City

Author: Asifiwe Mbembela