Bingwa wa mbio za London Marathon Daniel Wanjiru apigwa marufuku kwa kutumia dawa za kusisimua misuli

Mkenya Daniel Wanjiru, bingwa wa mbio za London Marathon mwaka 2017 amepigwa marufuku kushiriki riadha hadi mwaka 2023 kwa kosa la kutumia dawa za kusimumua misuli. Awali, Wanjiru alipigwa marufuku kwa muda hadi Aprili lakini amekanusha madai kwamba alitumia dawa zilizopigwa marufuku michezoni kuomba kufungua kesi mahakamani.

Shirika la kupambana na matumizi ya madawa ya kusisimua misuli duniani (AIU) sasa limethibitisha kwamba marufuku ya mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 28 itaendelea hadi Desemba 8, 2023.

Msimamizi wa Wanjiru amesema wamekatishwa tamaa na uamuzi huo na wanafikiria kukata rufaa kupitia mahakama ya usuluhishi wa mizozo katika michezo.

Author: Bruce Amani