Bocco, Gomes wakimbiza tuzo binafsi VPL

John Raphael Bocco amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Juni wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21, huku kocha Didier Gomes wa timu hiyo akichaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi huo.

Bocco ambaye ni nahodha wa Simba na Gomes wametwaa tuzo hizo baada ya kuwashinda wenzao waliongia nao fainali kwa mwezi Juni katika uchambuzi uliofanywa juma hili na kamati ya tuzo za VPL, kutokana na mapendekezo ya makocha waliopo vituo mbalimbali ambavyo Ligi hiyo inachezwa.
Strika huyo wa zamani wa Azam Fc alionyesha kiwango cha kizuri na kuisaidia timu yake kutwaa taji msimu huu kwa kuifungia mabao matatu akiwashinda nyota wawili alioingia nao fainali ambao ni Feisal Salum (Yanga) na Idd Seleman Nado (Azam Fc).
Hii ni mara ya pili Bocco kutwaa tuzo hiyo baada ya mwezi Novemba mwaka jana, kwa mwezi Juni Simba ilizifunga Ruvu Shooting 0-3, Polisi Tanzania 0-1 na Mbeya City 1-4.
Kwa upande wa kocha Gomes aliwashinda Naserddin Nabi (Yanga) na George Leandamina (Azam Fc), ambapo kocha huyo wa Simba aliiongoza timu yake kushinda michezo yote mitatu ndani ya mwezi huo.
Wachezaji wengine ambao tayari wameshatwaa tuzo hiyo ya mwezi kwa msimu huu ni Prince Dube wa Azam FC (Septemba) na Mukoko Tonombe wa Young Africans (Oktoba), John, Bocco (Novemba), Saido Ntibazonkiza (Desemba), Deogratiu Mafie Biashara (Januari),
Makocha waliotwaa tuzo hiyo ni Aristica Cioaba aliekua Azam FC (Septemba) na Cedrick Kaze wa Young Africans (Oktoba).
Wakati huohuo kamati ya tuzo imemchagua meneja wa uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Jonathan Mkumba kuwa mshindi wa meneja bora wa mwezi Juni. Meneja huyo ameibuka kuwa mshindi baada ya kufanya vizuri kwenye menejimenti ya michezo iliyochezwa kwenye uwanja huo.
TFF imekua na utaratibu wa kutoa tuzo ya mchezaji bora na kocha bora wa VPL kila mwezi, ambapo pia mwisho wa msimu kunakua na tuzo za wachezaji mbalimbali waliofanya vizuri, kwa msimu mzima ikiwemo tuzo ya mchezaj bora wa Tanzania.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares