Bodi ya Ligi yampiga mkwara Bernard Morrison, Simba wapewa adhabu

Kamati ya Uendeshwaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Tanzania Bara (TPLB) imepitia matukio mbalimbali yaliyotokea viwanjani na kutoa maamuzi, ambapo kwenye mechi baina ya Mwadui Fc dhidi ya Simba winga wa Simba Bernard Morrison amepewa onyo kali.

Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Bodi ya Ligi imesema kamati hiyo imejidhihirisha kwa ushaidi kuwa kitendo alichofanya Morrison hakikubaliki michezoni kama ambavyo mwamuzi alimpa kadi ya njano, kama sehemu ya onyo.
Hata hivyo, Kamati hiyo imetoa onyo kali kwa mchezaji yeyote mwenye vitendo kama hivyo.
Mbali na onyo, klabu ya Simba imepigwa faini ya shilingi laki tano (500,000) kama faini kufuatia mashabiki wa timu hiyo kurusha chupa za maji kwenye mechi dhidi ya Gwambina Fc, mtanange uliomalizika kwa Simba kushinda goli 1-0.
Mlinzi wa Simba pia amefungiwa mechi tatu na faini ya shilingi laki tano kutokana na kumuzuia mwamuzi kutofanya kazi yake katika mechi ya Simba na Gwambina.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares