Bondia Mayweather kugharamia mazishi ya George Floyd Mmarekani mweusi aliyeuliwa na mzungu

Bondia na mshindi wa zamani wa mataji ya uzito wa juu wa ndondi Floyd Mayweather, 43, amejitolea kulipia gharama zote za mazishi ya George Floyd ambaye aliuawa na polisi aliyemdhibiti vikali katika Mji wa Minneapolis.

Waandamaji nchini Marekani wameendelea kupinga mauaji hayo huku ulimwengu pia ukiwa macho na kuwa sehemu ya wanaopinga ukatali kwa watu wenye asili ya Afrika ambao umekuwa ukifanyika nchini humo na maeneo mengine duniani.

Licha ya kufutwa kazi kwa polisi Derek Chauvin aliyefanya mauaji hayo, bado maandamano yamekuwa yakiendelea siku hata siku.

Ripoti mbalimbali kutoka nchini Marekani zinasema familia ya Floyd imekubali ofa hiyo, ambapo mazishi yatafanyika Houston katika maeneo ya Minnesota na Charlotte katika maeneo ambayo marehemu George alikuwa anaishi.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends