Bondia wa Marekani afariki dunia baada ya kuumia ulingoni

Bondia Patrick Day amekutwa na umauti siku nne tangu ashuke ulingoni dhidi ya mpinzani wake Charles Cornwell akisumbuliwa na majeraha ya Ubongo. Day, 27, alikuwa katika uangalizi maalumu tangu Jumamosi alipomaliza pambano lake la uzito wa juu huku akipoteza kwa KO katika raundi ya 10 ya mchezo, Chicago.

Promota Lou DiBella alithibitisha jana Jumatano kutokea kwa kifo cha mwajiri wake. Patrick Day katika uhai wake alishinda mapambano 17 kati ya 22 huku akipigwa mapambano manne na kutoa droo pambano moja.

Kifo cha Day kinakuwa kifo cha tatu kwa Wanandondi ndani ya muda mfupi ambapo mwezi Julai Mrusi Maxim Dadashev na Hugo Santillan raia wa Argentina wote walipoteza uhai kutokana na majeraha waliyoyapata wakiwa ulingoni.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends