Bordeaux yaiwekea kikomo rekodi ya PSG

Paris St-Germain iliangusha pointi kwa mara ya kwanza msimu huu katika ligi kuu ya kandanda Ufaransa – Ligue 1 baada ya kutoka sare ya 2-2 na Bordeaux.

Sare hiyo pia ilikuja kwa gharama baada ya Neymar kuumia katika mechi hiyo. Nyota huyo wa Brazil alifunga bao la kwanza kutokana na krosi ya Dani Alves lakini akaondoka uwanjani na maumivu ya misuli ya paja. Jimmy Briand alisawazisha lakini Kylian Mbappe akaiweka PSG kifua mbele kutokana na pasi ya Julian Draxler.

Andreas Cornelius alifunga bao la dakika za mwisho mwisho na kuisawazishia Bordeaux na hivyo kuiwekea kikomo rekodi ya PSG kushinda mechi 14 mfululizo kwenye ligi tangu mwanzo wa msimu

Hata hivyo bado PSG wanaongoza ligi na pengo la pointi 14 mbele ya nambari mbili Montpellier.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments