Borussia Dortmund wawawekea presha vinara Bayern Munich kwa kuwabwaga Wolfsburg

Mabingwa wa Bundesliga mwaka 2012 Borussia Dortmund wameendelea kuipa hofu ya kuendelea kutawala soka la Ujerumani Bayern Munich hasa ikichagizwa na kuelekea kwa mtanange wa Jumanne baina ya timu hizo kubwa Ujerumani.

Borrusia Dortmund ambao leo Jumamosi walikuwa ugenini wamefanikiwa kuichapa bila huruma Wolfsburg goli 2-0 katika mtanange ambao umeendelea kukosa mashabiki kutokana na janga la virusi vya Corona ambapo mashabiki wataendelea kukosekana mpaka mwishoni mwa msimu huu.

Munich inapata presha kwa sababu endapo watapoteza hata mchezo mmoja kati ya iliyosalia huenda basi Dortmund ikaipiku na kuongoza mpaka tamati.

Ushindi wa goli mbili ulianza baada ya Raphael Guerreiro kufunga goli la kwanza na goli la 8 kwa msimu huu akimalizia mpira wa Thorgan Hazard, hata hivyo Dortmund ambao wanakamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa Bundesliga walipata goli la pili kupitia kwa Achraf Hakimi akimalizia pasi ya Jadon Sancho.

Ushindi wa leo wa Dortmund unamaanisha kuwa wamefikisha pointi 57 wakizidiwa alama moja na Bayern Munich ambayo ina alama 58 kabla ya kucheza dhidi ya Eintracht Frankfurt. Bayern hata hivyo walishuka dimbani na kuwachbanga Eintracht Frankfurt 5 – 2 na kurejesha pengo la pointi nne kileleni.

Matokeo mengine kwenye Bundesliga ni pamoja na

Paderborn 1-1 Hoffenheim

Borrusia Monchengladbach 1-3 Bayer Leverkusen

Freiburg 0- 1 Werder Bremen

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends