Bosi wa Bayern Hoeness apuuza uvumi kuhusu usajili wa Sane

Juhudi  za  Bayern Munich za kupata saini  ya  mshambuliaji  wa  Manchester City Leroy Sane  zinaonekana  kugonga  mwamba, rais  wa  klabu  hiyo Uli Hoeness amenukuliwa  akisema  katika  ripoti Jumatatu.

“Unalazimika  kuwa  kidogo  na  shaka. Kuna  uwezekano  kwamba  haitawezekana. Ni  kuhusu wenda  wazimu  wa malipo ya  uhamisho,” gazeti  la  michezo  la  Kicker  lilimnukuu Hoeness. Kwa  mujibu wa  ripoti  za  vyombo  vya  habari, Manchester City inafanya  juhudi  mpya  kurefusha  mkataba  wa  mchezaji  huyo  wa  kimataifa  wa  Ujerumani  mwenye  umri  wa  miaka  23.

Author: Bruce Amani