Brazil yatoa kichapo cha 4-2 kwa Ujerumani Olimpiki Tokyo 2020

Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil na Everton Richarlison ameisaidia timu ya taifa kushinda bao 4-2 dhidi ya Ujerumani katika mchezo wa kwanza wa Olimpiki Tokyo 2020 uliopigwa Leo Alhamis.

 

Goli tatu ambazo Richarlison amezifunga kwenye mchezo huo zimeandikisha rekodi ya kuwa hat-trick ya kwanza katika taaluma yake ngazi ya taifa.

 

Mechi hiyo ukiwa kama ukumbusho wa mtanange wa 2016 wa Olimpiki ulishuhudia Brazil kuongoza licha ya penati kuokolewa na Matheus Cunha.

 

Richarlison alifunga kutokea kwenye mpira wa kujirudi kabla ya kuongeza bao la pili na la tatu ndani ya dakika 30 za awali, baada ya mapumziko Ujerumani walibadilika ambapo walipata bao 2 za haraka kupitia kwa Nadiem Amiri na Ragnar Ache.

 

Hata hivyo nyota wa Bayer Leverkusen Paulinho alimaliza mchezo kwa kufunga goli maridhawa kwenye muda wa jioni na kufanya matokeo kuwa 4-2.

 

Kwenye kundi D, kiungo wa AC Milan Franck Kessie ametupia wakati Ivory Coast ikishinda bao 2-1 dhidi ya Saudi Arabia.

 

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares